Kenya ilipata uhuru
kutoka Uingereza mwaka wa elfu moja sitini na tatu na ikawa jamuhuri
mwaka ifuatayo
Kenya ina ardhi
tofauti tofauti. Kuna sehemu zimekauka na sehemu zinazo faa kwa ukulima.
Hali ya anga pia ina tofautika kulingana na geographia ya sehemu fulani,
na misimu ya mvua au ukame. Kuna baridi na mvua nyingi miezi za Aprili
hadi Augusti , na jua kali na joto jingi miezi hizo zingine.
Kenya ina makundi ya
watu wenye tabaka na lugha mbali mbali. Lugha ya taifa ni Kiswahili na
Kiingereza. Idadi ya watu Kenya imekaribia milioni thelathini, na
uongezeko wa watu umekuwa ukipungua.
Kenya ina miji mingi na
mji mkuu ni Nairobi. Eldoret ni mji moja wa Kenya. inapatikana upande wa
magharibi kwenye ikweta. Eldoret ina hali nzuri ya hewa mwaka nzima na
ardhi nzuri kwa ukulima na ufugaji wa wanyama, na kwa hivyo imezungukwa
na mashamba mengi.
Hear this
page read in Swahili, click the controller button.